UONGOZI wa Klabu ya Simba umemtangaza Haji Sunday Manara kuwa ofisa habari mpya kwenye klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Katibu Mkuu wa Simba, Stephene Ally alisema kuwa ofisa habari huyo ameteuliwa na kamati ya utendaji baada ya kuona anakidhi vigezo.
Stephene amesema, aliyekuwa ofisa wa timu hiyo, Humphrey Nyasio yeye amebadilishiwa majukumu katika sekretarieti ya Simba katika kuhakikisha wanafikia malengo yao.
“Uongozi kwa jumla umelipitisha jina la Manara kuwa ofisa habari wetu katika klabu yetu ya Simba na Nyasio aliyekuwa ofisa habari yetu tumembadilishia majukumu mengine,” alisema Stephene.
Post a Comment