Idadi
ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko ya mvua ya mawe iliyonyesha
katika kata ya mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeongezeka na
kufikia watu 46 huku idadi ya majeruhii waliopelekwa hospitali ikipungua
baada ya kutibiwa na kuruhusiwa kuondoka.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la msalala Ezekiah maige
wakati akizungumza katika mahojiano maaalum kabla ya kumpokea
waziri mkuu ambapo amesema kati ya majeruhi 91 wanne wamepoteza maisha
na kufikia idadi ya vifo hadi sasa kuwa 46.
Akitoa taarifa ya serikali waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera
uratibu na bunge Mh. Jenista Mhagama amesema serikali ipo tayari
kuhudumia waathirika kwa misaada mbalimbali ikiwemo chakula na vifaa
muhimu na kuwataka kamati ya maafa mkoa ihamishie ofisi za uratibu
katika eneo la tukio ili waathirika wapate huduma kwa wakati.
Akitoa rambirambi za serikali waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema
serikali imekuja na timu ya waratibu watakaoratibu mahitaji kwa
waathirika ili waweze kusaidiwa kwa kutumia ghala la chakula la kanda
lililoko shinyanga kutoa chakula na hakuna atakayekosa chakula.
Baadhi ya waathrika wameeleza pigo walilopata kwa kuondokewa na
ndugu katika familia zao pamoja na kuachwa bila hata makazi ya kuishi
achilia mbali mashamba kufagiliwa na mvua hiyo hatari ya upepo na mawe.
chanzo:itv
Post a Comment