Mama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jana jioni alizungumza na kituo cha runinga cha Taifa, TBC na kukanusha uvumi ulioenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameaga dunia.
Akizungumza na mtangazaji, Mama Nyerere alimuuliza,
"ukiniangalia unanionaje?" ambapo mtangazaji alimjibu, "nakuona mzima!" huku
wakitabasamu.
Mama Maria alisema huu ni mwaka wa uchauguzi, hivyo
mambo haya ya uzushi si ya ajabu.
Kabla ya uvumi wa kizushi kuhusu Mama Maria, juzi
kupitia WhatsApp ulikuwa ukitumwa ujumbe mwingine wa kumzushia kifo Reginald
Mengi, Mwenyekiti wa makampuni ya IPP.
Bonyeza hiyo video hapo chini Umsikie mama Maria Nyerere.
Bonyeza hiyo video hapo chini Umsikie mama Maria Nyerere.
Mpekuzi blog
Post a Comment