Mbunge
wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akielezea maendeleo ya
ujenzi wa Shule ya msingi Lowasa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Muungano wilaya ya Chamwino mkoani
Dodoma.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana(kushoto) akimuonyesha Mbunge wa
Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde namna ya kufatua matofali
wakati wa kushiriki ujenzi wa shule ya msingi Lowasa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupampu maji ya kisima
cha mkono kilichopo katika shule ya msingi Mvumi Mission mara baada ya
kukagua na kuuzindua mradi huo wa maji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi.
Happiness Misile ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule mara baada ya
kuzindua kisima cha maji katika shule ya Msingi Mvumi Mission.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi mara baada
ya kuzindua kisima cha maji ambapo aliwaambia wananchi hao watunze
sana miundo mbinu ya maji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Suli kata ya Mvumi Makulu ambapo alijionea ujenzi wa shule ya Msingi
Suli unavyoendelea.
Mkuu
wa Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Farida Mgomi akimwagilia maji mti
alioupanda katika shule ya Sekondari ya FUFU ikiwa sehemu ya utunzaji
mazingira.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Fufu Hassan M.Kilindi kwa kuweza kujenga
bweni zuri la wasichana shuleni hapo.
Mbunge
wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akicheza ngoma wakati wa
kuwasili kwenye uwanja wa mkutano wa hadhara uliofanyika Manzase.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akijadiliana jambo na
Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde (kushoto) na
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chamwino Ndugu Charles Ulanga kabla ya
kuhutubia wakazi wa Manzase.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Chamwino akisalimia wananchi wa Manzase.
Mbunge
wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusindeakihutubia wakazi wa Manzase
ambapo aliwaambia kuwa watendaji wa Serikali wajitahidi kufuata maagizo
na maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa wakati.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Manzase na
kuwaambia CCM Ipo Imara inajenga nchi na kuwataadharisha vijana
wasikimbilie vyama visivyo na sera za maendeleo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Manzase
wilaya ya Chamwino na kwenye mkutano wa hadhara wa CCM ikiwa sehemu ya
ziara yake ya kukagua, kusisitiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
mwaka 2010.
Wazee wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kinana.
Wananchi wa Manzase wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati
akihutubia wakazi wa Manzase ambapo pia aliwasisitiza kujiandikisha kwa
ajili ya kupiga kura.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi ya uanachama wa
CCM kwa Bi.Roda ambapo zaidi ya wanachama wapaya 750 walijiunga na CCM.
Katibu Mkuu akiwashukuru wazee wa Manzase mara baada ya mkutano kuisha.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) pamoja na Mbunge wa
Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde wakiwashukuru wananchi mara
baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Manzase,wilaya ya Chamwino.
on Tuesday, March 10, 2015
Post a Comment