Kiungo Ivan Rakitic amekuwa shujaa kwa kufunga bao pekee katika mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora kati ya wenyeji Barcelona dhidi ya Manchester City.
Barcelona imesonga hadi robo fainali baada ya kupata ushindi ikiwa nyumbani hivyo kuvuka kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya ushindi wa 2-1 ikiwa ugenini.
Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi alikuwa katika kiwango cha juu, kwani licha ya kutoa pasi ya bao, lakini ndiye alikuwa akiwapa wakati mgumu mabeki na viungo wa City hadi “mzee mzima” yaya Toure, akatolewa.
Naye Sergio Aguero alikosa penalti iliyopatikana baada ya yeye kuangushwa.
VIKOSI:
Barcelona: Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mathieu, Jordi Alba, Rakitic, Mascherano, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar.
Subs: Bravo, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Sergi Roberto, Adriano.
Subs: Bravo, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Sergi Roberto, Adriano.
Man City: Hart, Sagna, Kompany, Demichelis, Kolarov, Nasri, Toure, Fernandinho, Milner, Silva, Aguero.
Subs: Caballero, Zabaleta, Fernando, Dzeko, Bony, Jesus Navas, Lampard.
Subs: Caballero, Zabaleta, Fernando, Dzeko, Bony, Jesus Navas, Lampard.
CREDIT: Salehe Jembe
Post a Comment