Mwanamke mmoja mkazi wa manispaa ya Shinyanga amejifungua mtoto wa ajabu wa kike asiyekuwa na mdomo wala pua huku masikio yake yakiwa shingoni katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema mtoto huyo alizaliwa jana saa moja asubuhi na alifariki muda mfupi baadaye kutokana na kasoro alizokuwa nazo.
Mwandishi wa habari Nunu Abdul amefuatilia kwa ukaribu zaidi habari hii,Tutawaletea habari kamili hivi punde,ikiwemo sababu za kuzaliwa kwa watoto wa namna hiyo.
Credit: Malunde1 Blog
Post a Comment