Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za rapa nchini Afrika Kusini Nkululeko Habedi ameuawa baada ya kugombana na mpenzi wake wa kike.
Mdogo
wa mwanamuziki huyo alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa
alimuona kaka yake anapoteza maisha kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Ndugu
wa mwanamuziki huyo ambao walishuhudia tukio hilo wamesema kuwa
waliamka mapema kuelekea kwa kaka yao na baada ya kufika karibu na
nyumba yake walisikia kelele zikitoka ndani, muda mfupi walimuona rapa
huyo akiwa anatokwa na damu nyingi kutokana na kugombana na mpenzi wake
kwa muda wa masaa mawili.
Polisi nchini humo wamesema kuwa mpenzi wake huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hizi ni baadhi ya kutoka eneo la tukio:
Watu wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye eneo la tukio
Post a Comment