Mechi
namba 117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa,
imeingiza jumla ya Sh milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya
watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.Watazamaji 309
walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa
(Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia
watazamaji 36,693.
Mgawanyo
wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh.
17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.
Mgao wa
Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya
Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh.
11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata
sh.81,727.83.
Wakati
huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne katika
uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro
watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.
Siku ya
jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji
wa timu ya Azam FC.
Aidha
mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) barani Afrika kati ya Young Africans
dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili
Machi 15, 2015 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA, BARAKA KIZUGUTO.
Post a Comment