Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anna Makinda amesema anamtambua Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zubeir Kabwe kuwa ni mbunge halali kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa rasmi kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusiana na ubunge wake kutenguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge Spika Makinda amesema kuna taratibu zilitakiwa kufuatwa ambapo mpaka sasa taratibu hizo hazijakamilika na kumfanya kumtambua kuwa ni mbunge halali wa jimbo hilo la Kigoma Kaskazini
Post a Comment