Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa meneja wa msanii Kajala,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki Samaki,Posta,jijini Dar.
Katika tukio hilo habari zinasema kuwa Shilole alikuwa
amelewa sana na kwamba walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh Mziwanda,ghafla
sehemu aliyokuwa amekaa Nuh na wasanii wengine ilirushwa chupa ambayo ilikuwa
ikimlenga msanii huyo bahati nzuri aliikwepa ikampiga jamaa mmoja lakini
haikumjeruhi.
Baada ya tukio hilo ilibidi baadhi ya wasanii wamuijie
juu Shilole na kumuuliza kwanini alitaka kumpasua Nuh kwa chupa,Shilole
alianzisha ugomvi na kuzua tafrani kwenye sherehe hiyo baadaye aliamua kukaa
pembeni peke yake na kuanza kulia.
‘’Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh sasa
hivi tungekuwa tunaongea mengine alikuwa anamjeruhi vibaya sana kiukweli alileta
fujo sana kwenye ile sherehe,"alisema mmoja ya watu walikuwa kwenye sherehe
hiyo.
Baada ya hapo msanii Quick Racka alimfuata Shilole na
kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo aliamka na kumrushia chupa
ambayo kwa bahati nzuri Quick Racka naye aliikwepa ikapasuka
chini.
Hata hivyo Soudy Brown kupitia Uheard alipompigia simu
Shilole kumsomea mashtaka hayo alimwambia asimsumbue kwani kwa muda huo alikuwa
amelala.
Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake
Nuh Mziwanda kwa kumpiga hadharani mara kwa mara ambapo miezi ya hivi karibuni
alimpiga vibao kwenye tamasha moja lililofanyika pande za viwanja vya Leaders na
baadaye kumuomba msamaha mpenzi wake kupitia vyombo vya habari na kuahidi
kutompiga tena.
Post a Comment