Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akianza mazoezi wakati akishiriki katika bonanza la Jogging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Jogging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
. Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gongo Gongo la Mboto kupitia Kipawa na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga ujumbe mkuu wa Bonanza hilo ulikuwa ni kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura kuliko kuwa mashabiki tu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu akiendelea na mazoezi wakati akishiriki Mazoezi katika bonanza la Joging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Joging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura . Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gonga Gongo la Mboto kupitia Kipawa na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga, Kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida
Wakiendelea na mazoezi hayo.
Makundi mbalimbali ya Jogging kutoka mkoa wa Dar es salaam yakishiriki katika mazoezi hayo.
Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na mazoezi hayo katika maeneo ya Kipawa pamoja navijana na watoto wadogo kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike,
Mazoezi yakiwa yapepamba moto eneo la uwanja wa Ndege
Kinana akifurahia jambo na watoto katika mazoezi hayo huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida kulia akimuangalia.
Makundi mbalimbali ya vilabu vya Jogging mkoa wa Dar es salaam yakiwasili katika viwanja vya Social Sitaki Shari Ukonga.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongoza Mazoezi hayo kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga.
Msanii wa musiki wa Mchiriku Maarufu kama Mkaanga Sumu akitumbuiza katika bonanza hilo.
Mratibu wa bonanza hilo Bw.Msafiri akizungumza na vijana waliojitokeza kwa wingi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanakulia akifurahia jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakizungumza na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
Dogo Asley wa Yamoto Band ya Mkubwa na Wanawe akifanya vitu vyake jukwaani katika bonanza hilo.
Kundi zima la Yamoto Bandi likifunika kwa shoo kali katika bonanza hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha na pamoja na vijana wa klabu ya Kaza Moyo Jogging Club mara baada ya kushiriki katika bonanza lao, Kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo Ndugu George Mtambalike.
Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotoa wito kwa tume ya uchaguzi kuhakikisha wanawahamasisha vijana ili kuiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura
Post a Comment