Zimesikika nyingi toka Kenya kuhusu ishu ya mashambulizi ya kigaidi.. leo kwenye zilizoripotiwa sio hiyo tena, hii inahusu vifo vya watu wanne, mmoja wao ni Askofu.
Mashuhuda wamesema watu hao wamefariki baada ya kula supu ya nyama ya ng’ombe ambayo wanahisi nyama hiyo ilikuwa na sumu, kati ya waliofariki yupo muuzaji pia wa supu hiyo.
Watu wengine sita ni majeruhi ambao bado wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali.
Maafisa Usalama wa Afya wamesema watu hao walikula chakula mahali ambapo sio salama, wakafanya msako na kumakamata watu ambao wanauza nyama bila kibali cha kufanya biashara hiyo.
Post a Comment