Baada ya picha chafu za Shilole kusambaa mtandaoni hadi kupelekea BASATA kumuandikia barua ya onyo, muimbaji huyo wa ‘Nakomaa na Jiji’ amevunja ukimya.
Shilole amesema kuwa hata yeye hakupenda kile kilichotokea jukwaani wakati akitumbuiza Ubelgiji hivi karibuni, kwa sababu ilikuwa bahati mbaya na hakudhamiria kukaa uchi kama wengi wanavyosema.
Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili amesema kuwa nguo mpya aliyoivaa siku hiyo ndio ilimponza kwasababu hakuwa ameifanyia majaribio ya kutumbuiza akiwa ameivaa.
“Kiukweli kwasababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwasababu ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri […] yaani hii nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati niko kwenye performance, ilitatuka wakati niko kwenye motion .” Alisema Shishi kupitia 255 ya Clouds Fm.
Ameongeza kuwa amesikitishwa na mtu aliyempiga picha hizo na kuamua kuzisambaza mtandaoni bila kujua kuwa itamuumiza yeye kama mwanamke.
“Nasisitiza tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi nitaunmia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje huyo mtu aliyefanya hivyo, sio mtu mzuri.”
Kuhusu kama amepokea barua ya kuitwa kujieleza kutoka BASATA, Shishi amesema kuwa hajapokea barua hiyo kwasababu bado yuko Ubelgiji
Post a Comment