"Kakaaaa ni wewe au Mimi mwaka huu..." Ni kama Pinda na Lowassa nateta juu ya Uchaguzi Mkuu 2015. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo na Waziri Mkuu, Mstaafu, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Monduli, Edward Lowassa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 19, 2015.
Viongozi hawa wote wawili wapo katika orodha ya wanasiasa wa Tanzania ambao wanasemwa na wawananchi kutaka kugombea urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka huu.
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa huenda akatangaza nia yake hiyo baadae mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na hii ni kufuatia makundi mbalimbali katika jamii kumtaka afanye hivyo.
Post a Comment