JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Namba ya simu 2502572 S. L.260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 25.06.2015.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
· MTU MMOJA MKAZI WA MBALIZI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA
MTU MMOJA MKAZI WA CHALANGWA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOFREY MWAMBONA @ ANKI (28) AMEKUTWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA KUTOLEWA KOROMEO.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UMETELEKEZWA KANDO YA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA MNAMO TAREHE 24.06.2015 MAJIRA YA SAA 23:59 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHALANGWA, KATA YA CHALANGWA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA AMETOKA GEREZANI HIVI KARIBUNI ALIPOKUWA AKITUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUBAKA WATOTO WATATU NA ALIKUWA AMETOKA KWA RUFAA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MSAKO UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
TAARIFA ZA MISAKO:
MTU MMOJA MKAZI WA MBALIZI NJE KIDOGO YA JIJI LA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUSAJO MWAMPOSA (29) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI (GONGO) UJAZO WA LITA 12.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 24.06.2015 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO MTAA WA NDOLA, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA UPIKAJI/UUZAJI WA POMBE HIYO ILI WAKAMATWE NA HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment