Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mfanyakazi wa Clouds atiwa mbaroni kwa utapeli



Aliyekuwa mfanyakazi wa Clouds Media, Cynthia Maximillan, amejikuta akitiwa mbaroni kwa madai ya kutapeli mamilioni ya shilingi ya wafanyakazi wenzake na marafiki aliosoma nao.
 
Inadaiwa kuwa mrembo huyo alitiwa rumande kituo cha polisi Oysterbay, baada ya kuwakusanya marafiki zake na kuwapa mchongo kuwa, kuna viwanja vinapatikana huko Bagamoyo kwa shilingi mil 1.5 kupitia Chama cha Mazingira Fukayosi.
 
Inasemekana kuwa baada ya kupewa fedha hizo mrembo huyo alianza kuwaletea habari ambazo walikuwa hawazielewi na ndipo wakachukua uamuzi wa kumshtaki kwa utapeli wake.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Clouds, Ruge Mutahaba, amedai kuwa anaomba umma ujue kuwa mrembo huyo sio mfanyakazi tena wa kampuni hiyo kwani aliachishwa kazi na yeye pia ni mhanga wa utapeli huo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top