Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS KIKWETE AREJEA NYUMBANI BAADA YA KUKAMILISHA ZIARA YA KIKAZI YA USWISI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mara baada ya kurejea nyumbani baada ya ziara ya kikazi mjini Geneva. PICHA NA IKULU

Akiwa mjini Geneva, Rais Kikwete ameongoza vikao vya  Jopo la Kimataifa Linalopendekeza Jinsi Dunia inavyoweza kukabiliana na majanga yajayo ya magonjwa ya milipuko ambalo kazi yake imeungwa mkono na nchi 21 ambazo zilichangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

Miongoni mwa mikutano ambayo Rais Kikwete ameiongoza katika Makao ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva ni pamoja na yeye na wanajopo wenzake kutoa maelezo kuhusu maendeleo ya kazi yao kwa nchi ambazo zilichangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Nchi hizo ambazo zimeunga mkono kazi ya Jopo hili katika mkutano huo ni Venezuela, Umoja wa Ulaya (EU), Uholanzi, Finland, Shirikisho la Russia (Russian Federation), Norway, China, Ubelgiji, India, Ujerumani, Marekani, Uswisi, Canada, Brazil, Denmark, Uingereza, Israel, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Umoja wa Afrika (AU), Benki ya Dunia (WB), Jamhuri ya Korea na Japan.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top