Mkuu
wa usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam, Peter Sima katikati
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Maonesho ya
usalama barabarani ya yatakayofanyika tarehe Agosti 24 na 25 mwaka huu
katika viwanja vya mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kulia ni
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi na Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni,
Awadhi Haji na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani,
Elifadhili Mgonja.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani, Elifadhili Mgonja.
Picha na Emmanue Massaka.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
AJALI
za barabarani jijini la Dar es Salaam zimepungua katika kipindi cha nusu
ya kwanza ya 2015 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa 2014.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti
wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Dar es Salaam, Elifadhili Mgonja
amesema kuwa takwimu zinaonyesha kupungua kwa ajali za barabarani 2,731
katika kipindi cha Januari -Juni 2015 zilitokea ajali za vifo 1,731
ikilinganishwa na ajali 4,462 zilizotokea kipindi cha Januari-Juni ,2014
ambayo ni sawa na upungufu wa asilimia 61.
Amesema kuwa ajali za vifo 87 katika kipindi cha Januari hadi juni
mwaka 2015 zimeripotiwa kwa ajali za vifo 165 ikilinganishwa na ajali
za vifo 252 zilizotokea katika mwaka uliopita ambayo sawa na asilimia
34.5.
Mgonja amesema idadi ya watu waliokufa 93 kwa 2015 katika na
idadi ya ajali zilizokuwa 187 kwa ikilinganishwa na watu waliofariki
280 katika mwaka uliopita sawa na asilimia 33.2.
Amesema upungufu waliojeruhiwa 1, 801 kwani mwaka huu
,waliojeruhiwa walikuwa 1,650 ukilinganishwa na mwaka uliopita wa mwaka
2014 uliokuwa na majeruhi 3,451 sawa na asilimia 52.18.
Aidha amesema kuwa wataandhimisha wiki ya usalama barabarani mkoa
wa Dar es Salaam kuanzia Agasti 24 hadi 28 katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Post a Comment