Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma,Antony Mavunde akionesha fomu
alizochukua za kugombea Ubunge katika jimbo hilo nje ya ofisi za
Halmashauri ya Dodoma.
Mgombea wa nafasi ya
Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Antony Mavunde akipungia mamia ya
mashabiki wakati akielekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Dodoma kwekuchukua fomu.
Mavunde akifurahia jambo na Wafuasi wake.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi,Antony Mavunde akikabidhiwa fomu na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Elizabeth Gumbo jana Mjini Dodoma.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi,Antony Mavunde akikabidhiwa fomu na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Elizabeth Gumbo jana Mjini Dodoma.
MGOMBEA wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM)Anthony Mavunde amechukua fomu na kuahidi kuwa mstari wa
mbele katika kuhakikisha analinda haki za wakazi wa mji wa Dodoma katika
masuala ya ardhi.
Akizungumza na wanachi mara
baada ya kuchukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Mavunde amesema
akipata nafasi ya kuwa mbunge kupitia nafasi hiyo atakuwa mjumbe wa
bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA)hivyo atahakikisha
mamlaka hiyo inaboresha maisha ya watu na sio kuyadidimiza.
Aidha
ameahidi kuimarisha sekta ya michezo ambayo imepewa kisogo katika Mkoa
wa Dodoma.Michezo hiyo
ni Pamoja na Mpira wa pete,Kikapu,Mpira wa mikono na Riadha.,Mavunde
alisema kama akipewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi
suala la michezo kwake litakuwa ni la lazima na inapiga hatua.
"Mimi ni muumini wa michezo hivyo tofauti na soka nitatoa nafasi pia
kwa michezo mingine ambayo imekuwa ikiipa sifa mkoa wa Dodoma ili vijana
waweze kujikwamua na kuondokana na tatizo la ajira, "alisema
Alisema akipata nafasi ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi cha kwanza
atakachofanya ni kukutana na viongozi wote wa vyama vya michezo mkoani
hapa ili kuweka kalenda za kisasa ambazo zitaendeleza michezo.
Mavunde alisema lengo lake lingine ni kuanzisha academic ya michezo
ambayo itakuwa ikiwaandaa vijana jinsi ya kuwa wachezaji wa kulipwa
katika miaka ya baadae pamoja na kuwatafutia soko la kwenda kuonyesha
vipaji vyao nje ya Tanzania.
Post a Comment