Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) lamvua ukamanda Kinguge Ngombale Mwiru


Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM lililokutana tarehe 15.08.2015 katika ukumbi wa Julius Nyerere International convention centre, pamoja na mambo mengine liliazimia mambo yafutauo:-
1. Lilimvua Ukamanda Mkuu ndugu Kingunge Ngombale Mwiru. Maamuzi hayo yalitolewa kutokana na tabia na mwenendo wake wa hivi karibuni kuenda tofauti na maadili na taratibu za CCM.
Aidha kikao kimetoa mapendekezo kwa vikao vya Chama Cha Mapinduzi kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.
2. Kikao pia kiliunda timu ya kampeni ambayo itafanya kazi pamoja na kamati ya utekelezaji kuhakisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.
3. Kikao kimemshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa Baraza na kikao kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo.
Sixtus Raphael Mapunda Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top