KAMBI kuu ya upinzani katika siasa za Tanzania, imezidi kuimarika. Matukio mawili, moja la jana, jingine leo hii, yametokea na kuongeza nguvu ya kampeni ya kuitoa CCM madarakani chini ya kaulimbiu ya “Toroka uje.”
Katika
tukio la kwanza jana jioni, kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) ilimpokea Omari Ayubu Kimbau, kada machachari wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), akihamia Chama cha Wananchi (CUF) anakotarajia kupewa
dhamana ya kugombea ubunge jimboni Mafia, Mkoa wa Pwani.
Kimbau
ni mmoja wa watoto wa Kanali Ayubu Shomari Mohamed Kimbau, mwanasiasa
mstaafu aliyekuwa mbunge wa muda mrefu wilayani Mafia.
Uamuzi
wa Kimbau kuhama CCM umefanikishwa mara tu alipobaini kudhulumiwa
kisiasa kulikotimia juzi kwa kutupwa nje ya mbio za uteuzi ka mara ya
pili mfululizo, ili kugombea ubunge.
Tayari
mipango ya kumkabidhisha bendera ya kugombea kiti hicho kupitia CUF,
inakamilishwa na taarifa za ndani ya CUF zinasema atatambulishwa rasmi
jimboni Jumatano wiki ijayo.
Kimbau
amekosa uteuzi katika vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC-CCM) vilivyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, ambako
ugombeaji alipewa Mbaraka Dau, ndugu wa damu wa Dk. Ramadhan Dau,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Katika
kura za maoni zilizohusisha matawi ya CCM jimboni, Kimbau alipata kura
1,480 huku Dau anayeishi Dubai, kwa shughuli za biashara, akipata kura
2,620. Injinia Omari Kipanga alipata kura 1,156; Shah 568 na Njalale 23.
Jimbo
la Mafia ambalo Abdulkarim Shah (Bulji) ameliwakilisha vipindi viwili,
kwa makubaliano ya UKAWA, limeachwa ligombewe na mwakilishi atokaye CUF,
chama chenye historia ya kuwa ngome kwa CCM wilayani Mafia.
Wachambuzi
wa siasa za Mafia, wanasema Kimbau ameingia kambi ya UKAWA akiwa na
mtaji wa zaidi ya wanachama 6,900 waliohakikiwa kujiunga Chadema kufikia
sasa; CUF zaidi ya 6,000; watu 1,480 waliompigia kura za maoni CCM.
Tukio
la pili ni la jijini Arusha ambako mgombea urais anayewakilisha UKAWA,
Edward Lowassa, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara wa kutambulishwa na
kupata wadhamini, ametinga kambini Lawrance Masha.
Masha,
waziri wa mambo ya ndani kwa awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Jakaya
Kikwete (Novemba 2005/2010), alipigwa kumbo katika uchaguzi mkuu
uliopita, jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza analowakilisha Ezekiel
Wenje.
“Maamuzi magumu yamefanyika hivi leo, lakini ni maamuzi muhimu sitaongea leo. Nitangaze tu kwamba nimejiunga rasmi Chadema,” amewaambia wana-UKAWA waliojazana viwanja vya Tindigani.
Masha
ni mtoto wa Dk. Fortunatus Masha, aliyestaafu siasa akiwa Chama cha
United Democratic Party (UDP) alikofikia ngazi ya makamu mwenyekiti.
Amehama
CCM siku chache baada ya kuthibitisha kutupwa na CCM katika uteuzi
kutokana na kushindwa kura za maoni safari hii akiwinda jimbo la
Sengerema.
Baada
ya mkutano wa Arusha, Lowassa, ambaye alihama CCM tarehe 28 Julai
akijibu pigo la kukatwa jina katika walioomba uteuzi wa kugombea urais,
akiwa miongoni mwa waombaji 38, atakuwa jijini Mwanza kesho Jumapili.
Post a Comment