Balozi
Mdogo wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika hafla fupi ya
kuwaaga wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China hafla iliyofanyika
ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa
Sycilia Temu wakati wa kuwaaga wanafunzi 78 wanaokwenda kusoma nchini
China kwa ufadhili wa nchi ya China jijini Dar es Salaam jana.
Balozi
Mdogo wa China nchini, Zhang Biao akizungumza na mwakilishi wa mkuu wa
chuo cha Kiislam cha Morogoro,Faraji Tamim katika hafla fupi ya kuwaanga
wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China iliyofanyika ubalozi wa china
jijini Dar es Salaam jana.
Mkufunzi
wa katika chuo cha Kiislamu cha Morogoro akiwa katika picha ya pamoja
na wanafunzi wa chuo cha Kiislamu cha Morogoro wanaoenda kusoma nchini
China.
Wanafunzi
wa Chuo cha Kiislamu cha Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa chuo kikuu wanaoenda kusoma nchini China.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKAILI
imesema kuwa wanafunzi waliopata ufadhili wa kusoma nchini China
wameweza kuleta mabadiliko nchini kutokana na kile ambacho wamekipata
kutumia katika sehemu mbalimbali za kitaaluma.
Hayo
aliyasema Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi,Profesa Sycilia Temu wakati wa kuwaaga wanafunzi 78 wanaokwenda
kusoma nchini China kwa ufadhili wa nchi hiyo,amesema waliopata
ufadhili wajitume na kuweza kuchangia mabadiliko katika Nyanja
mbalimbali ambazo zimewekwa kipaumbele na serikali.
Ufadhili
huo katika Chuo cha Kiislam Morogoro (MUM) wanafunzi waliopata ufadhili
ni 15 ambapo saba wanachukua uzalmili na saba watasomea Lugha ya
Kichina.
Profesa
, Sycilia amesema kuwa nchi ya China imepiga hatua kutokana na watu
wake kujituma hivyo wanaopata ufadhili wanatakiwa kufanya hivyo na
kuweza nchi kukua kiuchumi kutokana na elimu wanayoipata katika nchi
hiyo.
Aidha
amesema kuwa serikali ya China imekuwa ikitoa kipaumbele katika serikali
ya Tanzania kwa kutoa ufadhili hivyo kwa wale wanaopata watumie fursa
hiyo kwa kusoma kwa bidii kwani wahitaji wa ndani kutaka kusoma ni
wengi.
Kwa
upande wa Balozi Mdogo wa China nchini, Zhang Biao wanatambua
ushirikiano kati Tanzania na China na kuona kuna umhimu wa kusukuma
katika upande wa elimu kusoma na kuweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi
kam ilivyofanya nchi yao.
Amesema
hadi sasa wametoa ufadhili kwa wanafunzi 1500 katika ngazi ya uzalimili
na uzamivu ambapo wataendeleo kufadhili ili kuweza kufikia malengo
katika Nyanja mbalimbali.
Post a Comment