Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili kutano
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Anjela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza. Agrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wake.Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.Agrey
Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye
mkutano wa B, Samia Suluhu,[/caption] [caption id="attachment_61124"
align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai. Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Burudani
kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi
Mjini.[/caption] Na Joachim Mushi, Arusha CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha
mgambo wa halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa kamatakamata za
wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama pamoja na
vijana. Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea mwenza nafasi ya urais
tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara
katika mkutano uliofanyika uwanja wa Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na
kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na wananchi wengine.
Akinadi
ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa
akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni
marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za akinamama na vijana
wanaojitafutia ridhiki mjini. "...Iwapo CCM itafanikiwa kuingia mjini
naomba wale mgambo ambao uishi kwa kutegemea kukamata kamata bidhaa za
akinamama watafute kazi nyingine ya kufanyanya...hatutaki mgambo wa
kufanya kazi hizo ni marufuku,
"
alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu. Alisema Ilani ya CCM
imepanga kujenga viwanda vya kuchakata madini ili kuhakikisha vijana
wanapata ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na kufufua viwanda
vilivyosimama kikiwemo cha 'General Tyre' ikiwa ni mpango wa kumaliza
tatizo la ajira kwa vijana. Aidha alisema mpango mwingine ambao upo
kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia tatizo la mikataba ya ajira ya
madereva wa magari madogo na makubwa, "..
.Tukifanikiwa
kuingia Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya ajira ni kuhakikisha
inafanya kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira kwa madereva wa magari
madogo na makubwa," alisema Bi. Suluhu. Aliongeza Serikali ya CCM
itaunda ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji zinakuwa za uhakika
kwani Mkoa wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya watu inakuwa kila
uchao. Serikali ya CCM imepanga kushughulikia suala la rushwa na vitendo
vya ufisadi, uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka.
Awali kabla ya mkutano wa Arusha Bi. Suluhu alifanya mikutano katika
majimbo ya Hai, Siha na Arumeru yaliyopo mikoa ya Kilimanjaro kabla ya
kuingia Mkoani Arusha. Akiwa katika majimbo hayo mgombea aliinadi ilani
ya CCM pamoja na kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa CCM wa maeneo
hayo. Ambapo alisema Serikali ya CCM imepanga kuboresha huduma za afya,
elimu, uwezeshaji wa vijana na akinamama ikiwa ni pamoja na kutenga
shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya kuwainua akinamama na
vijana.
Post a Comment