Wakati
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akianguka katika
matokeo ya marudio ya kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Meya wa Ilala Jerry Silaa aliyemaliza muda wake ameibuka kidedea.
Dkt
Rashid alikuwa anatetea nafasi yake ya ubunge katika jimbo la Rufiji
dhidi ya mpinzani wake mkubwa Mohamed Mchengelwa, huku Silaa akiomba
ridhaa ya kuteuliwa na chama chake kuwania ubunge kwa mara ya kwanza
katika jimbo la Ukonga.
Katibu wa
CCM Wilaya ya Rufiji, Masililiyo Iriyo ameliambia Mwananchi Digital
toka Ikwiriri mkoani Pwani kuwa Mohamed Mchengelwa amemshinda Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid kwa kupata kura 6,002 sawa na
asilimia 51.1 ya kura halali 11, 738.
Iriyo alisema Waziri wa Afya, Dkt Seif Rashid alipata kura 5,010 sawa na asilimia 42.7 ya kura halali.
Hata
hivyo, taarifa toka Ikwiriri zinasema Dkt Rashid hakuwepo wakati matokeo
yanatangazwa, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wakisema huenda alipima
upepo na kubaini haukuwa unavuma vizuri kwa upande wake.
Jimboni
Ukonga, aliyekuwa Meya wa Ilala, Jerry Silaa amembwaga tena mrufani na
mpinzani wake wa karibu Ramesh Patel kwa kupata kura 10, 965 sawa na
asilimia 57.1 ya kura zote 19, 187 zilizopigwa.
Katibu wa
CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Charles ameiambia Mwananchi Digital kuwa
Ramesh Patel ambaye amekubali kushindwa kwa kusaini fomu maalumu za
chama hicho amepata kura 6, 960 sawa na asilimia 36.27.
Uchaguzi
katika majimbo hayo umefanyika baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM
kilichoketi mjini Dodoma hivi karibuni kuagiza urudiwe katika majimbo
matano yakiwemo Kilolo, Makete na Busega kutokana na dosari kadhaa.CHANZO:MWANANCHI
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON
Post a Comment