SASA ni
dhahiri kuwa mawaziri 11 wa Serikali ya Awamu ya Nne inayomaliza muda
wake, wametoswa katika mbio za kuwania ubunge kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kati yao wakiwemo watatu ambao kura katika majimbo yao
zilirudiwa baada ya kulalamikiwa.
Awali
katika kura za maoni za kupata wagombea ubunge wa CCM zilizofanyika nchi
nzima Agosti mosi mwaka huu, mawaziri tisa waliangushwa katika
kinyang’anyiro hicho, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (Nachingwea) na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundentia Kabaka
(Tarime Mjini).
Mbali na
hao, pia walikuwepo naibu mawaziri saba, akiwemo wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Pereira Ame Silima (Mambo
ya Ndani), Amos Makala (Maji), Kaika Saning’o ole Telele (Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi), Dk Makongoro Mahanga (Kazi na Ajira), Adam Malima
(Fedha) na Pindi Chana (Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto).
Baada ya
kura hizo za maoni, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM iliyokaa wiki
hii, ilibaini kuwepo kwa kasoro katika kura za maoni zilizofanyika
katika majimbo 11 ambako zililalamikiwa, yakiwemo matatu ya Busega
mkoani Shinyanga, Rufiji mkoani Pwani na Mahenge mkoani Iringa ambayo
yalikuwa yakiwaniwa na mawaziri watatu.(VICTOR)
Post a Comment