Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza
Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi
wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es
salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais
leo agosti 4, 2015.
Mhe
Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM
waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini
Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za
kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza
Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM
Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi
kuchukua Fomu za kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Picha ya pamoja
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi
wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John
Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama
hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na
Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt
John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia
chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi
Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan
Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura
za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe
Magufuli kuchukua fomu za kuwania Uraisi mapema leo jijini Dar.
Wafuasi
wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao
ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais
kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua
Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi
za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo
Wafuasi
wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi ndogo ya Makao
Makuu ya CCM mtaa Lumumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais
kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda
kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo
Shamra
shamra na vigele vigele vya wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM vikiwa
vimetawala nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumbumba
wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt
John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo
Gari
ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Jonh Pombe Magufuli
pamoja na Mgombea mwenza Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa tayari kwa ajili
ya kuwapeleka kuchukua fomu za kuwania Urais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha CCM,katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
jijini Dar leo.
Shamra shamra na vigele vigele vya wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM
vikiwa vimetawala nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM mtaa wa
Lumumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha
CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akitoka ndani ya ofisi za chama
hicho akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana
ichani kulia na viongozi wengine mbalimbali wa juu wa chama hicho
kulekea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu ya kuwania
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
Mgombea
Mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwa
kwenye gari la wazi akiwapungia mkono wananchi na wafuasi wa chama hicho
nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumumba wakishangilia
wakati Mgombea alipokuwa ikielekea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia chama hicho.
Dkt
Magufuli akiwapungia baadhi ya Wanachi hawapo pichani alipokuwa
akiwasili ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini
Dkt
John Magufuli akiwasalimia wananchi mara baada ya kuchukua fomu ya
kuwania urais kupitia chama cha CCM,katka Ofisi za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi jijini Dar leo.
Ilikuwa ni shangwe pia nje ya ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Wananchi wakirekodi msafara wa Dkt Magufuli
Baadhi ya Wananchi wakichukua matukio kwa simu.
Post a Comment