Mkutano Mkuu wa Chadema kwa pamoja umempitisha Mwanasiasa Edward Lowassa kama mgombea Urais na Juma Haji Duni kuwa mgombea Mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25 oktoba 2015.
Katika upigaji kura Kanda zote zimepiga kura ya NDIYO kwa Mh.
Edward Lowassa na hakuna kanda iliyosema HAPANA, huku wakishangilia kwa
nguvu.
Kanda ya Kaskazini, Kanda ya kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya
Kusini na nyingine zote pia zimepiga kura ya NDIYO kwa Juma Haji Duni
kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi nkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka
huu.
Kufuatia matokeo hayo Mwanasiasa Edward Lowassa atapambana na
Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja
na wagombea wengine akiwemo Mchungaji Christopher Mtikila wa chama cha
DP aliyechukua fomu ya urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(Nec) jijini Dar es salaam wiki iliyopita.
Post a Comment