Na Jenikisa Ndile
Idadi
ya wanafunzi wanaopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi
wa Elimu ya Juu (HESLB) imekuwa imeongezeka mwaka hadi mwaka na kusaidia
kuongeza idadi ya watanzania wanaopata elimu ya juu.
Katika
mwaka wa masomo wa 2005/2006 Bodi ya Mikopo ilitoa mikopo
kwa wanafunzi 42,729 iliyogharimu sh. bilioni 56.1 na mwaka wa masomo
wa 2014/2015 bodi ya mikopo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 98,000
iliyogharimu shilingi bilioni 345.
Hayo
yalisemawa leo na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na
Mawasiliano kutoka bodi hiyo Cosmas Mwaisobwa wakati akizungumza na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari
(MAELEZO) kuhusu mafanikio ya bodi hiyo katika kipindi hicho.
Alisema
kwa kipindi hicho chote wamekuwa na sheria mbalimbali ilioanzishwa kwa
kuwapa jukumu la ukusanyaji wa madeni ya mikopo ya wanafunzi wa elimu
ya juu ambayo ilianza kutolewa tangu mwaka 1994/1995 kupitia iliyokuwa
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati huo Serikali haikukusanya
madeni kutoka kwa wanufaika hadi pale bodi ilipoanza kazi rasmi mwaka
2006/2007.
Aliongeza
kuwa taasisi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kulinganisha na hapo
awali kwani kwa kipindi cha miaka kumi tumeongeza ufanisi katika
matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la
kuomba mikopo kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa uombaji wa mikopo wa
(OLAMS)
Aidha bodi
hiyo imeendelea kukua kwa kasi kutokana na idadi ya watumishi kutoka
tisa hadi kufikia watumishi 135 mwaka huu,ongezeko hilo limesaidia bodi
kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Bodi
hiyo imewawezesha wateja wake kupata huduma katika maeneo manne ambayo
ni Arusha, Mwanza, Dodoma, na Zanzibar ili kupata huduma za kibodi kwa
ukaribu zaidi.
Mwaisongwa aliwahakikishia
wateja hao wataendelea kuwanufaisha waombaji na kutambua kuwa mikopo
ya wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya
uchangiaji wa elimu ya juu na ni muhimu kurejesha mikopo ili kuwezesha
mfuko huo kuwa endelevu.
Taasisi
hiyo iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2004 na
kuanza rasmi julai 2005 yenye lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi i wa
elimu ya juu,utoaji na ukusanyaji wa mikopo ili kufanya mfuko wa mikopo
kuwa endelevu.
Post a Comment