Na Lilian Lundo, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete (Pichani)amezipongeza
sekta binafsi kwa kukubali kusaini hati ya ahadi ya uadilifu katika
harakati za mapambano dhidi ya rushwa na utovu wa nidhamu.
Rais
alisema hayo katika wakati akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa
hati hizo zinazojumuisha sekta ya Umma na Binafsi katika ukumbi wa
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika
hafla hiyo, Mhe. Rais alisaini hati tatu ambazo ni Hati ya ahadi ya
uadilifu ya Viongozi wa Umma, hati ya ahadi ya uadilifu ya Utumishi wa
Umma na hati ya uadilifu ya Sekta Binafsi.
“Ushiriki
wa sekta binafsi katika hati hii utasaidia kuleta mabadiliko ya kuwa na
mwenendo wa kimaadili ya mapambano dhidi ya rushwa” alisema Mhe.
Kikwete.
Rais
Kikwete alisema kuwa badala ya wananchi na sekta binafsi kulalamika
pembeni ni vyema kuwasilisha malalamiko yao katika sehemu husika ili
hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Aidha,
Rais aliongeza kuwa baadhi ya sekta binafsi zimekuwa zikiombwa na
kutoa rushwa ili kupewa upendeleo wa kupata tenda serikalini, hivyo
kwa kusaini hati hiyo ya ahadi ya uadilifu kutaondoa mianya
ya upokeaji na utoaji rushwa katika sekta hiyo.
Hati
ya ahadi ya uadilifu inakumbusha Makampuni, Viongozi na Watumishi wa
Umma juu ya wajibu wao wa kuzingatia kanuni za maadili na mapambano
dhidi ya rushwa nchini.
Wazo
la kuwa na ahadi ya uadilifu liliibuliwa katika maabara ya Mpango wa
Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambapo ilionekanakuwa rushwa
bado ni tatizo katika uendeshaji wa shughuli za Umma na Binafsi hususani
utoaji huduma kwa umma na biashara.
Post a Comment