Aliyekuwa
mgombea Urais wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama
hicho, Januari Makamba, jana alimshukia mgombea urais kwa tiketi ya
Ukawa, Edward Lowassa kwamba ni mroho wa madaraka.
Makamba
alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wakati akimnadi
mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde. January
alisema kuwa Lowassa ameivuruga demokrasia ndani ya Chadema na kupeleka
mizengwe itakayokiua chama hicho na umoja wao.
“Yale
siyo mabadiliko kama wanavyojinadi bali ni uroho wa madaraka kwa mtu
mwenye uroho na chama chenye uroho, lakini hawezi na hawawezi kushika
madaraka ya kuongoza nchi,” alisema Makamba.
Alisema
kinachoendelea kwa vyama vinavyounda Ukawa ni maigizo na siyo mabadiliko
ya kweli kwa sababu mgombea urais ametoka CCM na Sera za CCM na mgombea
mwenza ametoka CUF na sera za huko, hivyo hawawezi kuungana kwa pamoja
kwa sababu hawajui nini maana ya kile wanachogombea.
Hata
hivyo, Makamba alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu kuliko
uchaguzi wowote uliowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi na
akawataka wana CCM kujiandaa kikamilifu.
Alisema
CCM kinapaswa kuwa makini na imara wakati wote ili kutoyumba na
wakifanya hivyo watajikuta wanapata mchanganyiko ambao utaleta shida
katika maendeleo.
Kwa
upande wake mgombea ubunge Mavunde alijipachika jina la Mr Makao akisema
lazima ataipelekea Dodoma hadhi ya kweli katika kufikia makao ambayo
yamekuwa yakisemwa kama hisani.
Mavunde
aliomba wananchi kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwani ana uhakika kwa
miaka mitano ataifanya Dodoma kupaa kiuchumi huku akisema atashughulika
na watu wenye kipato cha chini pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi.
Chanzo:Mwananchi
Post a Comment