Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya
kauli zinazotolewa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (Ukawa), zinaashiria
uvunjifu wa amani pindi matokeo ya kura yatakapoanishwa baada ya zoezi
la upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.
Rais
Kikwete alisema baadhi ya kauli hizo zimekuwa zikionyesha wazi
viashiria vya uvunjifu wa amani na upotoshaji kwa kundi kubwa la vijana
ambao wanapiga kura kwa mara ya kwanza.
Akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao jijini Dar es Salaam Rais Kikwete alisema;
“Wamediriki
kusema wazi bila kificho kwamba patakuwa hapatoshi, hizi ni kauli
zinazoashiria uvunjifu wa amani. Tunachokisema CCM ushindi kwetu ni
lazima na tutashinda kwa kishindo na kwenda nginja nginja mpaka Ikulu.”
Kikwete
alisema CCM imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu
ujao na kuongeza kuwa ili kufanikisha hilo wamepanga kikosi kazi
ambacho kitatembea nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, mtu kwa mtu
ikiwa kwa sasa tayari wameshaanza kufanya kampeni zao kupitia mtandao ya
simu za mkononi.
Katika
hafla hiyo ya kuzindua kampeni hiyo inayoratibiwa na msanii wa filamu
na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Rais Kikwete aliwataka
wanawake kaungalia mazuri yote yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika
kumuinua mwanamke.
Post a Comment