BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza,
msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua
kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza
kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta, jijini Dar
kulipokuwa na fainali za Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo
washiriki 10 ndiyo walikuwa wakiwania kitita cha shilingi milioni 50.
Mara baada ya mshindi wa shindano hilo
kutangazwa, ukumbi mzima ulizizima kwa kelele za furaha na kwenda
kumpongeza Dennis Laswai aliyeibuka kidedea na wengi walikubaliana kuwa
ni haki yake kutokana na kufanya vizuri.
Ndipo ghafla, Ray ambaye alikuwa na
upinzani wa kisanii na muigizaji huyo, alipoanza kumwaga machozi
hadharani na kujikuta amezungukwa na watu wakimshangaa.
“Jamani mrithi wa Kanumba amepatikana
rasmi baada ya miaka mitatu kuishi bila yeye, sasa jembe limerejea tena,
mama yetu hapaswi kuwa na simanzi kila siku,” kijana mmoja alisikika
akisema huku akienda kumshika mkono mama Kanumba.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Ray baada
ya mmoja wa vijana hao kumfuata na kumuonesha fulana hiyo ambapo
alizidisha kilio kiasi cha wenzake kumfuata na kumtuliza ili awe katika
hali ya kawaida.
Mtu mmoja ukumbini hapo alibeza kilio
hicho, akisema hiyo yote ilitokana na kuzidisha ‘kiburudisho’ na wala
haikuwa kwa sababu ya kummiss sana marehemu kwani hawakuwahi kuwa na
ukaribu wa kiwango hicho.
“Ray hana lolote, pale amezidisha
kiburudisho tu, hakuwa na mapenzi na Kanumba kiasi hicho mpaka leo hii
alie vile, ni usanii tu hakuna lolote. Wapo watu wa kulizwa na kitu kama
kile na si yeye, halafu Ray huwa hana ushirikiano mzuri na wasanii
wenzie hasa wa kiume,” alisema mtu huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kwa upande wake Ray alisema kilichomtoa
machozi ni ukweli kwamba mshindi ana kipaji cha hali ya juu na yeye
binafsi alipenda ushindi wake kiasi kwamba mawazo yake yalimfikisha
mbali.


Post a Comment