Hatimaye Jeshi la Polisi Tanzania (PT) limeanika picha ya mtu
anayedaiwa kuwa ndiye mfadhili mkuu wa matukio mbalimbali yanayohusishwa
na ugaidi likiwemo lile la mauaji ya watu saba kwenye Kituo cha Polisi
Stakishari, Dar lililotokea saa 5 usiku, Julai 12, mwaka huu na yale
mapigano ya Amboni, Tanga.
Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la
Ally Mtozen Hery ambaye anadaiwa kuishi kwa kujibadili kama kinyonga kwa
muonekano wa sura, wakati mwingine huvaa mavazi ya kike ili asijulikane
kirahisi.
Akizungumza na Uwazi juzikati, Kamishna wa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi uliyofanywa na
kikosi kazi cha jeshi hilo umebaini kuwa, mtuhumiwa huyo ana mtandao
mpana na ndiye mfadhali mkuu wa matukio mbalimbali ya uvamizi,
mashambulio na uporaji wa silaha yanayotokea nchini.
Kova
aliongeza kuwa, hivi karibunim Hery amehusika katika kufadhili tukio la
Amboni Tanga, Mkuranga, Stakishari na mengineyo lakini hatimaye jeshi la
polisi kwa kutumia kikosi cha intelijensia kimeweza kubaini nyendo zake
na kuinasa picha yake hiyo.
“Tunachotaka mtu huyo ajitokeze mara
moja na kujisalimisha polisi. Kwani hata afanyaje lazima tutamkamata
tu,” alisema Kamishna Kova.
Akaongeza: “Ile milioni 50,000,000
iliyotangazwa na IGP Ernest Mangu sasa imefikia mahala pake kwa mtu
atakayeweza kusaidia kupatikana kwa mtuhumiwa huyo.”
Kova
aliendelea kusema mtuhumiwa huyo wakati mwingine hupenda kutembelea
Pemba, Tanga, Dar na ukanda mzima wa Pwani.Katika mahojiano na Kamishna
Kova alisema hadi sasa, watuhumiwa tisa wanashikiliwa na jeshi hilo
kutokana na tukio la Stakishari.
“Si vyema kuwataja kwa majina
tunaowashikilia kwa sababu za kiupelelezi lakini hadi sasa kwa jitihada
za jeshi letu makini tunawashikilia watuhumiwa tisa na mahojiano
yanaendelea,” alisema Kova.
Mbali na mtuhumiwa huyo kusakwa na
jeshi la polisi, mtuhumiwa mwingine aliyekuwa akisakwa na jeshi hilo
amejisalimisha polisi akiwa na wake zake wawili na sasa anahojiwa kwa
kina.
Aliongeza kusema mtuhumiwa huyo aliyejisalimisha polisi
aliwahi kuwa mtumishi ndani ya jeshi la polisi lakini alifukuzwa kazi
mwaka 1998 kutokana na kutoeleweka kwa nyendo zake.
Polisi huyo
aliyeachishwa kazi akiwa na cheo cha sajenti anafahamika kwa jina
maarufu la Mzee Mzima ambapo akiwa kazini kitengo cha redio (999)
ambacho hushughulikia matukio ya uhalifu kwa haraka nyendo zake zilikuwa
hazieleweki ndani ya jeshi hilo.
“Hatuwezi kuvumilia damu za
askari wetu zikipotea bure. Ni lazima tuhakikishe kazi tunaifanya
ipasavyo na hao watuhumiwa tisa tunaowashikilia wanaendelea kutupa
taarifa muhimu,” alisema Kova.
Loading...
Home » Unlabelled » Jeshi la Polisi Lamuweka Wazi Mfadhili wa Matukio Mbalimbali ya Kigaidi Tanzania
BLOG RAFIKI
-
-
-
Duniani Leo1 hour ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment