Wasanii wasitegemee msaada wa maana pindi Professor Jay akiingia
bungeni. Rapper huyo anayewania ubunge kwenye jimbo la Mikumi mkoani
Morogoro amesema atatumia wadhifa huo kuwahudumia wananchi wa Mikumi.
Professor
amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa atakuwa
mbunge wa watu wa Mikumi hivyo atatumia muda kuwatumikia watu wake.
“Nimewaambia
wasanii wangu na wanajua nimechaguliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA
kwenye jimbo la Mikumi, lakini wengi wamesema watanisaidia kwa maneno
lakini bado sijalaunch kampeni yangu rasmi. Natarajia kulaunch natarajia
rasmi tarehe 5 mwezi wa tisa, sasa tunaangalia nani atani-support,”
amesema.
“Mimi ni kijana na mimi ni mwanamuziki, watu waelewe
naingia bungeni kwenda kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Mikumi,
kwahiyo tutafanya kazi sawa za wananchi wa jimbo la Mikumi na Professor
atakuwa anaishi Mikumi na nitakuwa napatikana huko Mikumi.”
“Watu
wasitegemee nitaingia bungeni kwenda kuongea masuala ya wasanii sana
kuliko hata kuwawakilisha watu wa Mikumi. Watu wajue Professor Jay
atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi ni vile ni mwanamuziki nitapigania kwa
hali na mali maslahi ya muziki ili kuweka sanaa katika level za juu
zaidi.”
Loading...
Post a Comment