Mamia ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata mbalimbali za Tarafa ya Matombo , wilayani Morogoro, wakimlaki mgombea mteule wa chama hicho katika nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena ,( aliyeshika bahasha ) alipowasili Augosti 18,2015 eneo la Mtamba , Kata ya Kisemu, tarafa ya Matombo kwa ajili ya kupata wadhamini kwenye fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Mgombea
mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge Jimbo la
Morogoro Kusini, Prosper Mbena ( kushoto) ,akimwelekeza mwanachama wa
chama hicho, Mariselina Joseph , mkazi wa Kata ya Kisemu, tarafa ya
Matombo, wilaya ya Morogoro namna ya kujaza fomu ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ya udhanini wake , Augosti 18, 2015, Mbena ni Katibu wa Rais.
Mgombea
mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge Jimbo la
Morogoro Kusini, Prosper Mbena ( kushoto) ,akimwelekeza mwanachama wa
chama hicho, Mariselina Joseph , mkazi wa Kata ya Kisemu, tarafa ya
Matombo, wilaya ya Morogoro namna ya kujaza fomu ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ya udhanini wake
Katika hatua nyingine, mgombea
mteule wa chama hicho nafasi ya Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini,
Mbena leo ( Augosti 19) amerudisha fomu hizo katika Ofisi ya Msimamzi
wa Jimbo baada ya kukamilisha kwa kupata wadhamini wapatao 31 kutoka
Kata za Tarafa ya Matombo, Mvuha na Bwakila.
Pongezi kwa Prosper Mbena
Na John Nditi
MAMIA
ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata mbalimbali za
Tarafa ya Matombo Mvuha na Bwakila , wilayani Morogoro, wamejitokeza kwa
wingi kumlaki mgombea mteule wa chama hicho nafasi ya Ubunge Jimbo la
Morogoro Kusini, Prosper Mbena na udhamini katika fomu za ubunge za
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mgombea
Ubunge huyo kupitia CCM, alipokelewa na wanachama na wananchi wa
kawaida mpakani wa Jimbo hilo, darajani Ruvu na kusindikishwa na
pikipiki umbali wa kilometa 20 hadi eneo la makao makuu wa Kata ya
Kisemu, Mtamba .
Kabla
ya kudhaminiwa na wanachama wa Kata za Tarafa ya Matombo, Augosti 18,
mwaka huu, Mbena ambaye pia ni Katibu wa Rais, alitumia fursa hiyo
kuwashukuru wanaCCM kwa kumwamini na kupigia kura nyingi zilizomwezesha
kuongoza akiwa miongoni mwa wagombea sita wa Jimbo hilo.
Alisema
kutokana na wanachama kumwamini , amewaomba kuendelea kuunganisha nguvu
zao kwa kuwashirikisha mashabiki wa chama hicho kuweza kuwapingia
wagombea wa CCM katika nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais siku ya Oktoba
25, mwaka huu.
“
Tayari Chama kimewapata wateule wake kwa upande wa Udiwani, Ubunge na
Urais...sasa si wakati wa kuendeleza makundi bali kuyavunja na
kuunganisha nguvu tuwe timu moja ya ushindi wa CCM” alisema Mbena akiwa
katika Ofisi ya Kata ya Kisemu.
Alisema,
matatizo mengi ya Jimbo hilo anayafahamu kwa vile yenye ni mzaliwa na
mkazi wa Jimbo hilo , na aliyataja machache kuwa ni barabara za
pembezoni kutopitika na suala la maji, ajira kwa vijana na nyinginezo.
“
Nina mipango mingi ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa wananchi wa
Jimbo hili na nitayasema wakati wa kampeni za uchaguzi...kwani leo
nimekuja kwenu kuomba kupata udhamini wa fomu za ubunge za Tume
...hatujaanza kampeni , nitasema wakati huo” alisema Mbena.
Akiwa
Tarafa ya Mvuha na Bwakila kwa ajili ya kupata udhamini huo,
aliwatakawanachama wamwamini na kampeni zitakapoanza rasmi wamchangue
awe mbunge wao na kwamba moja na jukumu atakalolisimamia ni kukabiliana
na migogoro baina ya wakulima na wafugaji ili wananchi waweze kufanya
kazi za uzalishaji mali.
Alisema
, ni budi wafugaji na wakulima waishi kwa kuaminiana kila mmoja
amheshimu mwezake na kwamba dhuruma inapotendeka haki inakosekana .
“
Kila upande unamhitaji mwezake mkulima anamhitaji mfugaji na mfugaji
anamhitaji mkulima , tusipo heshimiana ndiyo dhuruma ipokuwa na kwa
maana hiyo mbunge hawezi kutetea dhuruma , lazima haki ndiyo itawale “
alisema Mbena.
Baadhi
ya wananchi wa Jimbo hilo, Iddi Selemani pamoja na Michael Pius, kwa
nyakati tofauti walisema, wamemchagua Mbena kwa kura nyingi za maoni
ndani ya chama wakitambua uwezo wake atakapokuwa mbunge kuweza kusimamia
maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
Naye
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Morogoro Vijijiji , Salum Jaza,
akizungumza kabla ya kukaribidha mbunge mteule wa chama katika Jimbo
hilo, alisema , wananchi wana matarajio yao ya kupata maendeleo na moja
ni kuwezesha kuwa na chuo cha ufundi stadi (VETA) ili kuwawezesha
wanafunzi wanaohitimu darasa la saba na sekondari za kata wapate ujuzi
wa ufundi wa aina mbalimbali ili wajiajiri wenyewe.
.
Alisema
, matatizo mengi ya jimbo hilo yanafahamika na hivyo atakapotapa ridhaa
ya kuwa mbunge , ni wajibu kuyapatoia ufumbuzi kwa kushirikiana na
wananchi wa jimbo hilo.
Post a Comment