Dkt. Jakaya Kikwete akiingiza
ufunguo wa trekta aliyozawadiwa na Bodi ya Wahandisi kama ishara ya
kumtakia maisha mema anapoelekea kupumzika.
Dkt. Kikwete akishuka katika trekta aliyopewa mara baada ya kukabidhiwa kwenye hafla hiyo.…
Dkt. Jakaya Kikwete akiingiza
ufunguo wa trekta aliyozawadiwa na Bodi ya Wahandisi kama ishara ya
kumtakia maisha mema anapoelekea kupumzika.
Dkt. Kikwete akishuka katika trekta aliyopewa mara baada ya kukabidhiwa kwenye hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) na Mgombea Urais 2015
Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya Pamoja na Wahandisi wa
Majengo.
Wanakamati wa maandalizi ya hafla hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Kikwete.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
leo ameagwa na wafanyakazi wahandishi jijini Dar es Salaam ikiwa ni
ishara ya kumtakia kila la heri kuelekea kumaliza kipindi chake cha
miaka 10 ya uongozi wake.Msajili wa Bodi ya Wahandisi Injinia Steven D.M Mlote, akisoma risala wakati wa hafla hiyo, alisema Bodi ya Usajili wa Wahandisi (Engineers Registration Bodi) iliundwa chini ya sheria ya Bunge Na.24 ya mwaka 2007, ikiwa na jukumu la kuratibu na kusimamia mienendo ya shughuli za kihandisi zinazofanywa na wahandisi pamoja na makampuni ya ushauri wa kihandisi nchini.
Alisema katika kipindi cha awamu ya nne, Bodi imeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kusajili wahandisi 8,496 kutoka 6,868 wa awali mwaka 2005 hadi kufikia 15,364 mwaka huu.
Alifafanua kuwa Bodi pia ilifanikwa kusajili makampuni ya ushauri wa kihandisi 160 na kufanya kuongeza kutoka 119 mwaka 2005 na kufikia 279 mwaka 2015.
Aidha, alisema idadi ya wahandisi wataalamu wanawake waliongezeka kutoka 39 mwaka 2005 hadi 298 kwa mwaka huu, hivyo jumla ya walisajiliwa kwa kipindi cha miaka kumi kuwa 259.
Mlote alisema kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015, Bodi ilikagua jumla ya miradi ya ujenzi 4,116 huku baadhi yake ikikiuka sheria hivyo hatua kali zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na kufuta usajili wa wahandisi 330 na makampuni 32 ya ushauri wa kihandisi.
Aidha pia Bodi ikisoama taariafa yake ilielezea pia changamoto inayoikumba Bodi ya Wahandisi kuwa ni pamoja na maslahi kuwa chini, hivyo baadhi ya wahadisi kuamua kuikimbia taaluma yao na kwenda kufanya kazi ambazo sio za kihandisi zinazodaiwa kuwalipa zaidi.
“Bodi ya Wahandisi hukabiliwa na changamoto ya maslahi kuwa chini na baadhi yao kuamua kuikimbia taaluma na kwenda kufanya kazi zingine zinazowalipa zaidi,” alisema Mlote.
(PICHA/ HABARI: DENIS MTIMA/GPL)
Post a Comment