MKAZI wa Kijiji cha Ishunju, wilayani Missenyi, Sikitu Filemoni (27), amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumsababishia mwenzake ulemavu wa kudumu.
Hukumu
hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Gera,
Allen Ifunya, ili iwe fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine
wanaoshindwa kutawala hasira zao.
Ilielezwa
mshitakiwa alimrukia Dafroza Severian (41), mkazi wa kijiji hicho na
kumng’ata mdomo, kitendo kilichosababisha kuondoa kipande cha mdomo wa
chini, hivyo kupata ulemavu wa kudumu.
Ilielezwa
mahakamani kuwa, Agosti 4 mwaka huu, wanawake hao walikuwa wakibishana
kuhusu matokeo ya kura ya maoni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
iliyofanyika Agosti Mosi, ikuhusu udiwani katika Kata ya Ishunju, ambapo
mgombea aliyekuwa akipendwa na mshitakiwa alishindwa, hivyo kujihisi
kuwa anazomewa na mwenzake, ndipo alipomrukia na kumng’ata.
Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikiri kutenda kosa hilo.
Hakimu
alimhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, adhabu itakayoanza
kutumikiwa baada ya kuthibitishwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya.
Katika
matokeo ya kura ya maoni ya udiwani kwenye kata hiyo, Msafiri Nyema
maarufu Matelefoni, aliibuka mshindi kwa kupata kura 477, akiwabwaga
Murshid Ibrahim (388) na Vincent Kamugisha (190).
Post a Comment