Akizungumza
na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya
kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho jana mchana, Lowassa
alisema;
“Rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”
“Rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”
“Wakati
Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni
Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh.
250 leo ni Sh. 1,200.”
Aidha
Lowassa alisema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo
na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika
historia ya Tanzania.
“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.
“Kila
aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi
yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi
akae pembeni,” alisema Lowassa na kuongeza:
"Nauchukia sana umaskini kama ugonjwa wa ukoma, dhamira yangu ni kwenda Ikulu ili kupambana nao kwa nguvu na akili zangu zote...katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, asilimia 72 ya vijana ndio watakaopiga kura hivyo naenda Ikulu kutengeneza Serikali.
"Serikali yangu itakuwa rafiki kwa waendesha pikipiki za bodaboda, mamalishe na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga hivyo tunzeni vichinjio vya kupigia kura (vitambulisho).
Angalia video hii hapo chini umsikie Lowassa akitoa tuhuma hizi.:-
Post a Comment