Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema anawatakia kila la heri wanaobeza nguvu ya umma.
Kutokana
na umati wa watu waliojitokeza jana kumlaki kuanzia Uwanja wa Ndege wa
Mwanza alikowasili saa saba mchana, iliuchukua zaidi ya saa mbili
msafara wake kuingia Viwanja vya Furahisha saa tisa alasiri, ambako ni
takriban kilomita nane.
Katika
hotuba yake iliyochukua dakika 14 kuanzia saa 11.53 hadi 12.07 jioni,
Lowassa alisema anawasikitikia wanaobeza nguvu hiyo ya umma.
“Haya siyo mapenzi, haya ni mahaba. Wanaobeza nguvu hii ya umma nawatakia kila la heri,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na umati huo.
Akizungumzia
idadi hiyo ya wananchi, mke wa mgombea huyo, Regina Lowassa alisema
haijawahi kutokea maeneo yote waliyotembelea Dar es Salaam, Mbeya na
Arusha.
“Mwanza nimewapenda, nafikiri baba (Lowassa) akitoka hapa atalala usingizi mzuri mzito,” alisema Regina.
Lowassa
aliwataka polisi kutoingilia mchakato wa uchaguzi na kutumiwa na CCM
kupambana na wapinzani na kwamba, wakiendelea watakuwa wanajitafutia
tiketi ya kupelekwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), mjini The
Hegue.
“Nimesikitishwa
sana kuwa watu wamepigwa mabomu asubuhi. Mkiendelea na mchezo huu
tukimaliza uchaguzi tutawapeleka The Hague mkakipate cha mtoto na huko
hamtarudi tena,” alisema.
Ampa Wenje kibarua
Lowassa
alisema ziara yake hiyo inahusu kujitambulisha na asingependa kuwapa
nafasi wapinzani wake kumtafsiri kuwa hajui sheria, lakini kero za
Mwanza anazifahamu hivyo akaahidi kurejea na mikakati ya kuzitatua.
Alisema
anafahamu Wamachinga, meli ya Mv Victoria, kiwanda kikubwa cha
kusindika nyama, reli, ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege, bei ndogo ya
pamba na tatizo la umeme.
Kuhusu
suala la umeme, Lowassa alisema Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje ni
kijana anayefanya uamuzi mgumu kama yeye hivyo alimtaka leo kwenda kwa
Meneja wa Tanesco Mwanza ili kujua tatizo, asipopewa majibu ya
kuridhisha ampigie simu yeye (Lowassa).
Freeman Mbowe
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mbowe, alisema nchi nzima kuna msiba wa umaskini kuanzia kwa watumishi wa umma, sekta binafsi, wakulima, wafugaji, wamachinga na mama lishe.
Hata hivyo, alisema msiba huo umesababishwa na kikundi kidogo cha viongozi wachache wanaotumia woga na umaskini huo kuendelea kuwakandamiza wananchi.
Alisema wananchi mkoani Mwanza waliojitokeza kumdhamini Lowassa na mgombea mwenza wake, Juma Haji Duni, ni zaidi ya 100,000, lakini waliojazwa kwenye fomu ni 200 kama kanuni na taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), zinavyotaka.
“Namwambia Mkuu wa Majeshi, asiliingize Jeshi la Wananchi wa Tanzania kusaidia ushindi wa CCM...vijana watatu wataalam wa kompyuta aliowachukua katika Jeshi la Wananchi na kuwapeleka Nec kwa majukumu maalum ambayo yataisha Novemba 15, amewapeleka kufanya nini?” alihoji.
Aliongeza kuwa: “Namuuliza Jaji Lubuva, hao vijana wa kijeshi uliowapokea ofisini kwako umewapokea kwa kazi gani?...nipo tayari kutoa ushahidi wa taarifa hizi.”
Alisema ana ushahidi wa namba, majina na vikosi wanavyotoka askari hao pamoja na tarehe waliyoanza kazi Nec.
Twaha Taslima
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Cuf, Twaha Taslima, alisema kwa mujibu wa sheria, polisi wanapaswa kulinda amani iliyopo na siyo kusababisha fujo kwa kuwapiga mabomu wananchi wanapokusanyika kwa amani.
James Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema polisi wakiendelea kutumia nguvu dhidi ya raia wasio na silaha, wataishia The Hague kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Novemba.
Alisema ilani ya Chadema chini ya mwavuli wa Ukawa itakayozungumzia malengo ya serikali ya awamu ya tano, itazinduliwa Jumamosi wiki hii sambamba na uzinduzi rasmi wa kampeni.

Post a Comment