Mgeni
rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd
Abdulmalik Mollel akuzungumza na wananchi juu ya Kuzuia kabisa mwendo
kasi kwa magari makubwa barabara ya kutoka bandarini kuelekea ubungo
kupitia ama Barabara ya Kilwa ama ile ya Mandela kwa wakati wote, na
kuweka msisitizo wa alama za mwendo kasi katika barabara hizo kwakuwa
pia imekuwa ikichangia kukosa umadhubuti wa breki pindi tatizo la ghafla
linapojitokeza, jana jiji Dar Salaam.
Sehemu
ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi Ambaye ni Mkurugenzi
wa Kmpuni ya A&T Brothers co.Ltd Abdulmalik Mollel jana katika
maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es
Salaam.
Wanafunzi
wakitoa maelekezo kwa wananchi jinsi ya kutumia vifaa maalum vya kuzuia
magari ili watembea kwa miguu wavuke barabara jana katika maadhimisho
ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd
Abdulmalik Mollel akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jana
katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usala ma Barabarani Kanda ya Dar
es Salaam.
Mrakibu
wa Jeshi la Polisi Chang'ombe Temeke akizungumza na waandishi wa habari
juu ya kupungua kwa ajali kwa kiasi kikubwa katika Manispa ya Temeke
jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara Kanda ya
Dar es Salaam.
Kaimu
Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke Thabit Massa
akizungumza na waandishi wa habari juu ya wananchi kutunza miundo mbinu
ya barabara jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama
Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd
Abdulmalik Mollel (mwenye suti nyeusi) akiwa pamoja na Kaimu Mwenyekiti
Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke Thabit Massa wakipatiwa
maelekezo na wanafunzi sehemu za makutano ya barabara zinazosababisha
ajali jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara
Kanda ya Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd
Abdulmalik Mollel akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Jeshi la
Polisi jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani
Kanda ya Dar es Salaam.
Mgeni
Rasmi Ambaye ni Mkurugenzi wa Kmpuni ya A&T Brothers co.Ltd
Abdulmalik Mollel na Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa
wa Temeke akianga marabaada maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama
Barabara Kanda ya Dar es Salaam Picha na Emmanuel Massaka.
---
HOTUBA YA MGENI RASMI UFUNGUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOA WA KIPOLISI WA TEMEKE. TAREHE 26/8/2015
Ndugu;
- Mkuu wa police Trafic mkoa wa Temeke (RTO). - Mwenyekiti usalama
barabarani ndugu -Thabit - Mkuu wa Operesheni – Temeke , Mr Mchuya -
Mkuu F.F.U – Mkoa polisi – Temeke - Ndugu kombe – mkuu wa kituo cha
polisi- Chang`ombe - Viongozi mbalimbali wa kipolisi mkoa wa Temeke -
Waalimu na wanafunzi wote mliohudhuria - Wadau wote mliohudhuria, mabibi
na mabwana – Itifaki imezingatiwa
Baada
ya kusikiliza na kuelewa kwa umakini changamoto mbalimbali zilizotolewa
na baraza la watoto la usalama mkoa wa Temeke, pia wadau wa usalama
barabarani ,yafuatayo naomba kuyarejea ili tuweze kuyapatia ufumbuzi wa
mara moja kulingana na uwezo wangu na kwa ushirikiano wa Polisi mkoa huu
na wadau wote kwa ujumla; Changamoto zinazosababisha kurudisha nyuma
jitihada za kupunguza ajali ni pamoja na zifuatazo:
1. Kutokuwa makini kwa madereva waendeshao vifaa vya moto .
2.
Kutokuwa na elimu ya kutosha ya alama za barabarani kwa watumiaji ambao
ni waenda kwa miguu au waendesha vyombo vya barabarani
3. Kutofuata alama za barabarani kwa watumiaji kama itakiwavyo
4.
Wasimamizi wa usalama barabarani kutokuwa makini hasa hatua zinapotakiwa
kuchukuliwa mara moja. Ndugu viongozi na wadau wote wa usalama mkoa huu
na Taifa kwa ujumla, Rekodi zinajionyesha ni kwa jinsi gani
tunavyopoteza ndugu na jamaa zetu kwa sababu ambazo
zinazuilika,ikizingatiwa kuwa hawa tunaowapoteza kwa ajali hizi ni moja
ya nguvu kazi ya Taifa hili.
Na
wadau wameomba serikali iweze kuchukua nafasi ya kupunguza ajali hizi
kwa kunusuru maisha ya watu, na hasa ikizingatiwa kauli mbiu ya mwaka
huu “ENDESHA SALAMA- OKOA MAISHA”.
Ndugu
wageni waalikwa, viongozi mbalimbali wa kipolisi,wanafunzi, waalimu na
waandishi wa habari, Ikumbukwe kuwa serikali ni sisi tulioko hapa kwa
kuwa ndio Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa nchi hii amewaamini
viongozi hawa walioko hapa kusimamia jukumu hili maalumu la usalama mkoa
huu wa Temeke.
Sina
hofu kabisa na (RTO) wa Mkoa huu, kwani Temeke imepunguza ajali kwa
asilimia hamsini (50%) kutoka 2014/2015 na hii inaonyesha jitihada na
mikakati madhubuti inayofanywa kama ambavyo chati imeonesha, Nami kwa
nafasi yangu kama mgeni rasmi leo, pia nikiwa mdau mkuu wa usafirishaji,
ninashauri viongozi wafanye yafuatayo,ikiwa pia nitakuwa mstari wa
mbele ktk kuhamasisha sekta binafsi zinazonihusu ili malengo yetu kwa
pamoja yaweze kufikiwa;
1.
Elimu itolewe mashuleni: Kikao cha wakuu wa shule, Afisa Elimu, Polisi
na wadau wengine kiitishwe mara moja, ili yapitishwe maazimio ya elimu
hii ya usalama barabarani, iwe ni yenye kutolewa kwa muendelezo katika
kipindi chao wawapo masomoni.
2.
Kiitishwe kikao cha wadau wa usafirishaji, viwanda,na watumiao vyombo
hivi vya moto watokao ktk eneo la kimkoa kipolisi Temeke, ili washiriki
katika kuchangia elimu hii kwa gharama za vitabu vyenye masomo hayo
vipatikane kwa wanafunzi.
3.
Vipindi vya siku za mpira uwanja wa Taifa: ninashauri muda wa kuanzia
jioni saa moja, magari yote yaliyoharibika njiani yasiachwe kabisa bila
kutolewa barabarani,
kwani
waendesha pikipiki huwa wanashindwa kuyaona kwa wakati na kusababisha
ajali zisizo na sababu na kuongezeka kwa vifo vya Raia wasiokuwa na
hatia.
4. Elimu katika makundi maalum: Iendelee kutolewa na kuthibitishwa kwa vyeti hasa waendesha bodaboda na magari makubwa.
5.
Mwendo Kasi:Kuzuia kabisa mwendo kasi kwa magari makubwa barabara ya
kutoka bandarini kuelekea ubungo kupitia ama Barabara ya Kilwa ama ile
ya Mandela kwa wakati wote,na kuweka msisitizo wa alama za mwendo kasi
katika barabara hizo kwakuwa pia imekuwa ikichangia kukosa umadhubuti wa
breki pindi tatizo la ghafla linapojitokeza,hivyo kupelekea ajali
kutoepukika.
6.
BREAKDOWN: Magari ya Breakdown yatumike kutoka polisi kwa zile gari
ambazo zitakuwa zimepata matatizo ya kiufundi,na kusababisha
uhatarishaji wa ajali kutokea,ziweze kuvutwa na kuwekwa nje ya eneo
hatarishi na hasa vipindi vya usiku unapokuwa umeingia.
Mwisho ninawashukuru wageni waalikwa, wadau wote waliowezakuitikia wito wa kongamano hili,na sasa ninatamka Rasmi’ Kongamano la Wiki ya Nenda Kwa Usalama limefunguliwa.’
Mwisho ninawashukuru wageni waalikwa, wadau wote waliowezakuitikia wito wa kongamano hili,na sasa ninatamka Rasmi’ Kongamano la Wiki ya Nenda Kwa Usalama limefunguliwa.’
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Temeke, ENDESHA SALAMA-OKOA MAISHA!!
Ni kwa ujenzi wa Taifa; Ndg. ABDULMALIK S. MOLLEL MGENI RASMI. A&T BROTHERS TRANSPORT CO.LTD
Post a Comment