MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amesema chama chake kinaandaa taratibu za kwenda mahakamani ili kumshtaki mgombea urais mteule wa CCM, Dkt. John Magufuli na mgombea urais wa CHADEMA, Bw. Edward Lowassa.
Alisema
wagombea hao kwa nyakati tofauti, wameshiriki kuiingizia Serikali
hasara ya mabilioni ya fedha ambapo wanasheria wa chama hicho wapo
katika hatua za mwisho ili wafunguliwe mashtaka mahakamani.
Mchungaji
Mtikila aliyasema hayo Dar es Salaam juzi, alipozungumza na waandishi
wa habari akisisitiza kuwa, wagombea hao wamepoteza sifa za kuwania
nafasi hiyo akidai hawana vigezo kwa mujibu wa sheria.
Aliongeza
kuwa, Bw. Lowassa, anahusishwa na sakata la kampuni ya Kufua Umeme ya
Richmond na kuishangaa CHADEMA akidai chama hicho kilipata umaarufu wa
kupinga vitendo vya ufisadi lakini wamempokea Bw. Lowassa ana tuhuma
kama hiyo.
"Kipindi
cha nyuma, CHADEMA walianzisha operesheni nyingi ikiwemo ya Sangara na
Movement for Change zikiwa na lengo la kupinga ufisadi, kwanini
wamempokea Lowassa waliyemuita fisadi.
"Hii
ina maana kuwa, ndani ya CHADEMA hakuna siasa, nawapongeza baadhi ya
viongozi wa chama hicho na wanachama wao ambao kimsingi hawakubaliani na
matakwa ya viongozi wa juu," alisema.
Akimzungumzia
Dkt. Magufuli, alimhusisha na tuhuma ya uuzwaji wa nyumba za Serikali
akidai kitendo hicho kimeisababishia hasara Serikali lakini hakupelekwa
mahakamani kwa kutumia madaraka yake vibaya kama ilivyokuwa kwa Basil
Mramba, Daniel Yona ambao hivi sasa wanatumikia kifungo gerezani.
Alisema
nyumba hizo zilikuwa makazi ya viongozi kama Majaji, Makatibu Wakuu na
Watendaji waandamizi serikalini ambao wengi wao walilazimika kuishi
hotelini kwa gharama za Serikali.
Post a Comment