Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IMEELEZWA kuwa Mtoto chini ya mwezi
hatakiwi kunywa maziwa yeyote isipokuwa ya mama yake, kutokana na maziwa ya
ng’ombe kuwa mazito na hayawezi kumsaidia
mtoto katika kukua kwake.
Hayo ameyasema mtaalam wa lishe wa Taasisi ya Chakula lishe
nchini (TFNC),Neema Joshua wakati wa semina ya waandishi wa habari ya
kuwajengea uwezo wa masuala ya Lishe,amesema maziwa ya ng’ombe wa yanatumika tu
pale hakuna namna ya kuweza kupata maziwa mengine.
Amesema watoto chini ya miezi sita
wanahitaji maziwa kwa mama na anatakiwa kupewa kila muda katika kuweza kumjenga
mtoto kiakili.
Neema amesema katika suala la
utapiamlo liko katika viwango vya juu ambapo mwaka 2010 ilikuwa na asilimia 42
hadi sasa imefikia asilimia 34.7 kwa takwimu za mwaka 2014.
Aidha amesema kuwa wale ambao
wananyonyesha wakapata mimba akiwa ananyonyesha anaweza kuuendelea kunyonyesha mtoto na bila kuathiri
mimba nyingine.
Amesema wakati akinyonyesha huku ana
mimba nyingine anatakiwa karibu na kujifungua miezi miwili aache kwa ajili ya
kuupa mwili nguvu kwa mtoto atakayezaliwa na baada ya hapo anaendelea
kunyonyesha wote wawili kwa kwanza akifikisha miwili ndipo anaweza kukoma.
Post a Comment