Naibu waziri maji akipokea maelezo kutoka kwa mhandisi Davis Fute kuhusu majitaka.
Naibu waziri maji akihutubia bodi na watumishi.
Mhandisi Stanley Mwasawale
akimweleza naibu waziri wa Maji ujenzi wa jengo la mamlaka ya maji
mwanza litakalogharimu shilingi bilioni 3.6
NAIBU
waziri wa maji Amos Makalla ametembelea Mamlaka ya maji jiji la Mwanza
kwa kutembelea chanzo cha maji, kituo cha kutibu maji, ujenzi wa jengo
la ofisi za mamlaka, mfumo wa majitaka na mkutano wa bodi na wafanyakaziKatika
mkutano na bodi na wafanyakazi amewataka kutoa huduma kwa wateja kwa
kiwango cha juu ikiwemo kusikiliza matatizo ya wateja na kuyashughulikia
kwa wakati.
Aidha
ameitaka menejimenti kuhakikisha mkandarasi wa kujenga mradi mkubwa wa
kuboresha huduma ya maji jiji la Mwanza hususan maeneo ya miinuko ananza
kazi novemba kama ilivyopangwa.
Mradi huo
mkubwa unagharimu shilingi bilioni 110 na ni ushirikiano wa serikali ya
Tanzania. Shirika la maendeleo la Ulaya na ufaransa
Kukamilika kwa mradi huu kutamaliza tatizo la maji jiji la Mwanza.
Post a Comment