Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Kikwete aongoza mazishi ya Peter Kisumo


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Kada Mkongwe wa CCM  Marehemu Mzee Peter Kisumo wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika huko kijijini kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo.
 .........................................................................................................
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Jakaya Kikwete jioni ya leo, ameungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya mwanasiasa mkongwe wa Tanzania,  Peter Kisumo ambaye amezikwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Ngujini, Wilaya ya Mwanza, Mkoa wa Kilimanjaro.
Akitokea Dodoma ambako amekuwa anaongoza vikao vya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Kikwete akifuatana na Mama Salma Kikwete, amejiunga na mamia ya waombolezaji wakati wa salamu zilizokuwa zinatolewa na watu mbali mbali katika Kanisa ya Usharika wa Kilindu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Mzee Peter Abdallah Kisumo ambaye alizaliwa Agosti Mosi, mwaka 1935 katika Wilaya ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro aliaga dunia Jumapili ya Agosti 2, mwaka huu, akiwa  na umri w miaka 80.
Wakati wa kutoa salamu, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha Rose Migiro ametoa kwa niaba ya Serikali na kwa niaba ya  Rais Kikwete, na Mzee David Cleopa Msuya ametoa shukutani kwa niaba ya familia ya Mzee Kisumo.
Mara baada ya kumalizika kwa salamu hizo kwenye Kanisa la Usharika wa Kilindu,  Rais Kikwete ameongozana na mwili wa marehemu ambao ulikuwa umepambwa kwa bendera ya CCM kwenda Kijijini Ngujini kwa mazishi. Mwili wa Marehemu Kisumo umeteremshwa kaburini kiasi cha saa 11:15 jioni.
    Mzee Kisumo ambaye alianza maisha yake ya kazi kama Bwana Shamba wa Serikali kabla ya kuingia katika uongozi wa vyama vya wafanyakazi alipata pia kuwa Waziri wa Serikali katika vipindi mbali mbali na Mkuu wa Mikoa ya Kilimanjaro (mara mbili), Singida, Pwani, Dar es Salaam na Mwanza.
 
Rais Kikwete ameondoka Kilimanjaro mara tu baada ya mzishi hayo kurejeaDodoma.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top