Wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali wakiwasili Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa
Kikosi namba 832 Ruvu JKT mkoani Pwani jana kwa ajili ya kujionea
shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Kikosi hicho kilichaguliwa
kuiwakilisha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuonyesha
mafanikio ya majeshi nchini katika shughuli mbalimbali zikiwemo za
uzalishaji mali ili kuinua uchumi wa taifa.
Mkuu
wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenelari, Jacob Gedion Kingu, alikuwa mgeni rasmi katika ziara hiyo ya
siku moja ya waandishi wa habari kutembelea kikosi hicho. Kingu
alimwakilisha Mkuu wa JKT nchini.
Mkuu
wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenelari, Jacob Gedion Kingu (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya
kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na kikosi hicho.
Mkuu
wa Kikosi 832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge, akizungumza na
waandishi wa habari wakati akimkaribisha Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu
kuzungumza na wanahabari katika ziara hiyo.
Mkuu
wa Kikosi 832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge (kushoto),
akiwaelekeza wanahabari wakati walipofika uwanja wa gwaride kuona vijana
wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wanavyofanya
mazoezi ya gwaride la kuhitimu mafunzo yao ya miezi sita mapema mwezi
ujao.Vijana wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wakionesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Mary
Raphael kutoka mkoani Singida mmoja wa vijana hao waliopo katika kambi
hiyo kwa mujibu wa sheria akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kuonyesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
January Sungura (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kuonesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Gelemaya Kibuga akizungumza na wanahabari.
Dk.
Meja Agustino Maile akiwaeleza wanahabari mambo yanafuatwa kabla ya
kumnyoa mteja katika saluni ya kisasa iliyopo katika kikosi hicho kwa
kuzingatia afya na kuepuka maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
Vijana wa mujibu wa sheria wakisubiri kunyolewa katika saluni hiyo.
Unyoaji katika saluni hiyo ukiendelea.
Rehama Hashim muuza wa duka katika kikosi hicho akiwaeleza wanahabari bidhaa zinazopatikana katika duka hilo.
Hapa ni eneo la kiwanda cha kushona nguo ambapo vijana wanaopitia jeshi hilo kwa mujibu wa sheria wanapata mafunzo.
Wanahabari
wakiangalia bweni lililojengwa kwa nguvu ya kikosi hicho kwa ajili ya
kukabilana na uhaba wa vyumba vya kulala vijana hao.
Wanahabari
wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Utawala na Mafunzo
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion
(katikati waliokaa mbele), pamoja na maofisa wa jeshi kutoka Makao Makuu
ya JKT na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Maofisa Habari
kutoka Idara ya Habari Maelezo.
Vijana hao wakipiga kwata mbele ya wanahabari na mgeni rasmi.
Vijana hao wakionesha onyesho la kuruka vikwazo.
Onyesho la kuruka vikwazo likiendelea.
Hapa wakiendelea kuruka vikwazo.
Ni Gwaride bila ya kutumia bunduki.
Wanahabari
wakiangalia Intaneti iliyojengwa kwa nguvu ya kikosini hicho kwa ajili
ya kusaidia wanafunzi kuona matokea yao pamoja na mambo mengine ya
masomo yao.
Vijana wakiwa katika intaneti hiyo.
Wanahabari wakiangalia mradi wa kuku wa nyama uliopo katika kikosi hicho.
Daktari wa Mifugo, Luteni Ezekiel Mtani (kushoto), akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu mradi wa kuku uliopo kikosini hapo.
Kuku wanaofugwa kikosini hapo wakiwa katika banda maalumu.
Wanahabari wakiangalia mabwawa ya samaki.
Msimamizi
wa mradi wa samaki katika kambi hiyo, Luteni Kelvin Ngodo (katikati),
akitoa maelezo ya mradi huo kwa waandishi wa habari.
Moja ya bwawa la samaki
Bwana
shamba wa kikosi hicho, Ndabemeye Ludovick Rwikima (kulia), akizungumza
na wanahabari kuhusu mradi wa shamba la matunda kikosini hapo.
Bata maji wanaofugwa kikosini hapo wakiwa kwenye banda lao.
Msimamizi wa mradi wa bata maji Rachel Muuta (kushoto), akitoa maelezo kwa wanahabari.
Kilimo cha Vitunguu si Ilula pekee hata Ruvu JKT kinafanyika. Vijana wa JKT wakipalilia vitunguu.
Msimamizi wa shamba la vitunguu, Koplo Robert Eliezer (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilimo cha vitunguu.
Utunzaji Mazingira. Wanahabari wakiangalia shamba la miti iliyipandwa na viongozi mbalimbali katika kikosi hicho.
Wanahabari wakiingia ulipo mradi wa usagishaji nafaka uliopo katika kikosi hicho.
Shughuli za usagishaji nafaka ukiendelea. usagishaji huo unafanywa na vijana wa JKT kwa mujibu wa sheria.
Wanahabari wakinagalia mradi wa usagishaji wa vyakula vya mifugo.
Burudani mbalimbali zikiendelea kutolewa na vijana hao.
Wanenguaji wa bendi ya JKT katika kikosi wakishambulia jukwaa.
Msemaji
wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Juma
Sipe, akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa ziara hiyo
ambapo aliwaomba wanahabari kuwa na ushirikiano na jeshi.
Mwakilishi
wa wanahabari hao, Mwanahabari Kibwana Dachi, akitoa neno la shukurani
baada ya kumalizika kwa ziara hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari
za jamii.com
Post a Comment