Rais wa
Simba Sport Club Evans Aveva wa tatu kutoka kushoto akiwa na Washindi wa
bahati nasibu Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup ImanKajula
kushoto na Msemaji wa Timu hiyo Manara.
Rais wa Simba Evans Aveva Akikabidhi Zawadi kwa Mmoja wa Washindi
Uongozi
wa klabu ya Simba leo umetoa zawadi kwa washindi wa bahati na sibu
iliyochezeshwa siku ya Simba Day Aosti 8 mwaka huu wakati wa kilele cha
sherehe za siku ya Simba Day zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Zawadi
zilizo kabidhiwa kwa washindi ni jezi pamoja simu, kila mshindi amepata
jezi ya juu pea moja pamoja na simu moja aina ya Motec. Washindi wa
zawadi hizo ni Jeremia Venist, Ahazi Mwembe pamoja na Marko Mgimba.(VICTOR)
Washindi wa bahati nasibu wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao
Mbali na
zawadi hizo, klabu hiyo pia imekabidhi mipira nane kwa shule mbili za
msingi za mkoa wa Dar es Salaam ambapo Shule ya Msingi Mikocheni A
imepata mipira minne huku Shule ya Mingi Chang’ombe Mazoezi nayo
ikikabidhiwa mipira minne.
Rais wa Simba Evans Aveva akimkabidhi mpira mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A
Rais wa
klabu ya Simba Evans Aveva amesema, klabu hiyo inataka kusaidia soka la
vijana nchini na kwasasa wameanza na mkoa wa Dar es Salaam lakini baadae
watasonga mbele hadi kwenye mikoa mingine ili kuwafikia watu wengi
zaidi hasa watoto ambapo ndio leno hasa la klabu hiyo kusaidia soka la
vijana.
Post a Comment