Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akizungumza na viongozi wa CUF pamoja na wagombea uwakilishi na ubunge
wa Chama hicho Wilaya za Unguja katika ukumbi wa majid Kiembe Samaki.
Viongozi
wa CUF pamoja na wagombea uwakilishi na ubunge wakimsikiliza Katibu Mkuu
wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad wakati akihutubia kwenye ukumbi
wa Majid Kiembesamaki.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu, akinukuu baadhi ya
vifungu vya katiba ya chama hicho vilivyoipa uhalali Kamati tendaji ya
chama hicho Taifa kufanya uteuzi ya wagombea katika majimbo
yaliyoongezwa kulingana na hali halisi ilivyokuwa.( VICTOR)
Katibu
Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi vifaa vya michezo
kwa viongozi wa wilaya na wagombea wa majimbo kama vitendea kazi vya
kampeni, ambapo kila jimbo lilikabidhiwa seti 40 za jezi na mipira 120.
Na Khamis Haji, (OMKR)
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wanancfhi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema
upepo wa kisiasa Zanzibar unakivumia vyema chama hicho na matarajio ni
kupata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kutokea wa asilimia 80
katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Maalim
Seif amesema hayo jana alipokuwa akiwahutubia viongozi wa Wilaya na
majimbo wa chama hicho huko Kiembesamaki, ambapo pia alitangaza timu
itakayo kiongoza chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi
mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.
Maalim
Seif amesema kwa namna wananchi wanavyokikubali chama hicho na namna
kilivyojipanga na iwapo kila kiongozi na mwanachama atatekeleza majukumu
yake bila ya kulalamika kitachukua idadi kubwa ya majimbo ya
uchaguzi na kushinda nafasi ya Urais kwa kishindo.
“Mazingira
yaliyopo Zanzibar ni mazuri sana kwa CUF kupata ushindi ambao haujawahi
kutokea, hivyo kila mmoja wetu aongozwe na dhamira ya kuchukua nchi
mwaka huu, na mara hii haibiwi mtu kura yoyote”, alisema Maalim Seif.
Alisema
malengo ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni kuwa na idadi ya
kutosha ya majimbo yatakayo kiwezesha kufanikisha kikamilifu mipango
yake ya kuwaletea matumaini na maisha bora Wazanzibari chini ya Serikali
ya Umoja wa Kitaifa.
Katika
mkutano huo ambao umehudhuriwa na wagombea waliopitishwa na chama kwa
upande wa Unguja, Maalim Seif amemtangaza Naibu Katibu Mkuu wa
CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui kuwa ndiye Meneja wa Kampeni za Urais
wa Zanzibar, akisaidiwa na mshauri wake wa Mikakati, Mansour Yussuf
Himid.
Aidha kwa
upande wa Pemba, Maalim Seif alisema Mratibu wa kampeni hizo ni Mjumbe
wa Baraza Kuu la Uongozi, Hamad Masoud Hamad akisaidiwa na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk.
Maalim
Seif alisema Zanzibar hakuna hata jimbo moja ambalo chama hicho kinaweza
kusema kwamba hakina matumaini ya kushinda na kwamba suala la kushinda
au kutoshinda litategemea chama hicho kimejipanga vipi kuchukua ushindi.
Katibu
Mkuu huyo wa CUF ameonya kuwa huu si wakati wa viongozi na wanachama
kuvutana na wala si wakati wa kukumbatia ubinafsi kwa baadhi yao kupeana
majukumu wasiyo yamudu kwa kwa kuzingatia urafiki au ujamaa.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu, Ismail Jussa Ladhu alisema CUF katika uchaguzi mkuu
wa mwaka huu CUF kitakuwa na kampeni ya aina yake kwa makusudi ya
kuwathibitishia Wazanzibari na nchi nzima kuwa kweli
kimejiandaa kuiongoza Zanzibar.
Jussa
alisema Agosti 22 wagombea wote waliopitishwa na chama kugombea
Uwakilishi watakwenda kuchukua fomu Tume ya Uchaguzi Zanzibar
kwa sherehe kubwa ili kila mtu apate habari kuwa safari ya chama hicho
kuiongoza Zanzibar na kutimiza matarajio yao i imezna rasmi.
“Siku hiyo wagombea wote wa Uwakilishi Zanzibar watakwenda
kuchukua fomu, mwenye kupiga dufu, mwenye kupiga mbwa kachoka, mwenye kupiga
rusha roho ni ruhusa kufanya sherehe hizo”, alisema Jussa.
kuchukua fomu, mwenye kupiga dufu, mwenye kupiga mbwa kachoka, mwenye kupiga
rusha roho ni ruhusa kufanya sherehe hizo”, alisema Jussa.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kwa upande wa nafasi ya Urais wa
Zanzibar, ambayo mgombea wake ni Maalim Seif Sharif Hamad
atakwenda kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo Agosti 23, ambapo pia
chama hicho kimeandaa shamra shamra za aina yake.
Katika
mkutano huo, Maalim Seif aliwakabidhi viongozi wa Wilaya na majimbo seti
40 za jezi kwa kila jimbo moja pamoja na mipira 120.
Post a Comment