Shirikisho la mpira wa miguu
nchini Tff imekiruhusu chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA
kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa chama cha soka wilaya
ya Temeke (TEFA) kama ulivyopangwa na kamati ya uchaguzi ya chama
hicho.
Baada ya ruhusa hiyo Uongozi wa
DRFA umemuandikia barua katibu wa TEFA Kasim Mustapha ili aijulishe
kamati ya uchaguzi ya chama hicho kuendelea na mchakato huo kama
kawaida.
Awali TFF iliiandikia barua DRFA
kushauri kusimamishwa kwa uchaguzi huo,kutokana na kile kinachoonekana
kuwepo na malalamiko kuhusu mchakato wake lakini maada ya mashauriano
kati ya pande hizo mbili,sasa ni ruksa kwa uchaguzi huo kufanyika kesho
jumapili Agosti 16,2015 kama ulivyopangwa.
Aidha DRFA imewaomba wapiga kura
wote kujitokeza kwenye uchaguzi,huku ikisisitiza amani na utulivu
itawale katika zoezi hilo muhimu la kuwapata viongozi watakaokiongoza
chama cha soka Temeke,ili kuleta maendeleo ya mpira wa miguu mkoa wa Dar
es salaam.
Post a Comment