MALINZI AMPONGEZA NDIKURIYO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundi (FBF) Reverien Ndikuriyo kwa
kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la Seneta nchini humo.
Katika salam hizo za pongezi kwa
Rais wa FBF na nakala zake kwenda CECAFA, CAF na FIFA, Malinzi ameelezea
imani yake kwa Seneta Ndikuriyo na amemtakia kila la kheri na mafanikio
katika nafasi hiyo mpya aliyochaguliwa.
TWIGA STARS YAENDELEA KUJIFUA ZANZIBAR
Kikosi cha timu ya Taifa ya
Wanawake (Twiga Stars) kilichoweka kambi kisiwani Zanzibar, kujiandaa na
fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) kimeendelea kujifua
kutwa mara mbili katika viwanja wa Aman na Fuoni kabla ya safari ya
kuelekea nchini Congo – Brazzavile mwezi ujao.
Twiga Stars chini ya kocha mkuu
Rogasian Kaijage inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa
ya Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23 katika uwanja wa Amani kisiwani
Zanzibari ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michezo ya hiyo ya Afrika
(All Africa Games).
Kaijage amesema anashukru vijana
wake wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu, wachezaji wanaonekana
kuyashika vizuri mafunzo yake na kumpa imani kuwa sasa kikosi chake
kimeiva na anachosubiri ni mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya ili kuweza
kuona uwezo wa kikosi chake kabla ya safari ya kuelekea nchini
Congo-Brazzavile.
Akiongeleaa maendeleo ya kambi ya
Twiga Stars, Mkuu wa Msafara Blassy Kiondo amesema timu ipo katika hali
nzuri, wachezaji wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu, hakuna
majeruhi kikubwa wanachosubiri kwa sasa ni huo mchezo wa kirafiki dhidi
ya Kenya mwishoni mwa wiki ijayo.
Post a Comment