Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana
hati ya makubaliano na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon
Kochanke (kushoto) katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta
za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es
Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kulia) akisaini
hati ya makubaliano katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta
za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es
Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon
Kochanke.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na baadhi ya
viongozi wa Wizara hiyo, ujumbe wa ulioandamana na Balozi wa Ujerumani
pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2
ya sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015)
Jijini Dar Es Salaam.(VICTOR)
Balozi wa
Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke akiongea na baadhi ya
viongozi wa Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na
waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za
maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es
Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akiteta jambo na
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke leo alhamisi
(Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini
wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili.
Baadhi ya
wajumbe wa ulioandamana na Balozi wa Ujerumani wakimsikiliza Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (hayupo pichani) alipokuwa
anaongea wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za
maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es
Salaam.
Baadhi ya
viongozi kutoka Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na
waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya
sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini
Dar Es Salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Serikali
ya Tanzania na Ujerumani zimetiliana saini mikataba miwili ya misaada
yenye thamani ya jumla ya Sh. Bilioni 39. 1 ambazo ni sawa na Euro
milioni 17 kusaidia sekta mbalimbali nchini.
Makubaliano
hayo yamesainiwa leo jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke ili kuleta mafanikio
na maendeleo katika.
Sekta zitakazonufaika na msaada huo uliotolewa na Serikali ya Ujerumani ni pamoja na sekta ya afya, maji na maliasili.
Aidha,
Dkt. Likwelile amemhakikishia Balozi Kochanke na ujumbe wake kuwa msaada
walioipa Serikali utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta
ufanisi na kuongeza nafasi za ajira na hatimaye kuchangia katika
kuboresha uchumi nchini.
Kwa
upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke amesema
kuwa serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa
kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Zaidi ya
hayo, serikali hizo mbili zimesaini mkataba wenye thamani ya Euro
milioni 10 ambazo ni sawa na bilioni 23 za kitanzania kuisaidia
usimamizi wa hifadhi ya taifa ya Selous.
Post a Comment